Pata taarifa kuu
OSLO-NORWAY

Mtuhumiwa wa mauaji nchini Norway kupandishwa kizimbani leo

Raia wa Norway Anders Behring Breivik anayetuhumiwa kutekeleza mauaji ya watu 92 katika matukio mawili tofauti ya mjini Oslo na visiwa vya Utoya, anatapandishwa kizimbani hii leo kujibu mashtaka yanayomkabili.

Anders Behring Breivik, mtuhumiwa wa mashambulizi ya Norway
Anders Behring Breivik, mtuhumiwa wa mashambulizi ya Norway Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria anayemtetea Breivik amesema kuwa ingawa mteja wake amekiri kuhusika na matukio yote mawili lakini anatarajiwa kukana mashtaka ya yeye kuwa muhalifu wakati atakaposomewa mashtaka katika mahakama kuu ya mjini Oslo.

Ulinzi umeimarishwa nje ya mahakama ambayo kesi hiyo itatajwa hii leo ambapo kumeripotiwa maelfu ya wananchi kukusanyika katika mahakama hiyo kutaka kusikiliza kile amabcho kinaendelea ingawa mahakama hiyo imepanga kusikiliza kesi hiyo katika mazingira ya usiri.

Breivik anatuhumiwa kuua watu saba mjini Oslo katika shambulio la bomu nje ya ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo na baadae alitekeleza mauaji mengine ya watu 85 katika visiwa vya Utoya ambako zaidi ya vijana 500 wa chama tawala nchini humo walikuwa wameandaliwa sherehe na chama chao na kuanza kuwapiga risasi.

Madaktari wanaowatibu watu waliojeruhiwa katika shambulio la risasi, wanasema kuwa mtuhumiwa alitumia risasi maalumu ambazi zilikuwa zikimpata mtu zinaharibu maeneo ya ndani ya mwili na hivyo kusababisha mtu aliyepigwa risasi hiyo kuwa katika uwezekano mdogo wa kupona jeraha.

Wakati huohuo polisi nchini humo kwa kushirikiana na wanajeshi wanaendelea na msako wa vijana wengine ambao hawajulikani walipo tangu tukio la kushambuliwa kwa risasi lilipotokea huku kukiwa hakuna matumaini ya kuwapata wakiwa hai.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.