Pata taarifa kuu
NORWAY

Majaji nchini Norway waamuru Breivik kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wakati uchunguzi ukiendelea

Majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya Anders Behring Breivik mtuhumiwa wa mashambulizi ya siku ya Ijumaa mjini Oslo na visiwa vya Utoya nchini Norway wameamuru mtuhumiwa huyo kuwekwa katika jela ya peke yake chini ya uangalizi maalumu. 

Anders Behring Breivik
Anders Behring Breivik REUTERS/Andrew Berwick via www.freak.no
Matangazo ya kibiashara

Upande wa mashtaka uliwasilisha maombi ya kuitaka mahakama, kutoruhusu mtuhumiwa huyo kuwekwa katika jela na wafungwa wengine wakitaka ahifadhiwe katika eneo maalumu peke yake chini ya Uangalizi wa Polisi.

Majaji hao walikubaliana na upande wa mashtaka wakisema kuwa mtuhumiwa huyo atakuwa akiruhusiwa kuonana na wakili wake peke yake na hataruhusiwa kupokea barua wala mgeni mwingine yeyote.

Mtuhumiwa huyo ametakiwa kuhifadhiwa katika jela maalumu peke yake kwa kipindi cha wiki nne za awali wakati uchunguzi ukiendelea.

Akihojiwa mahakamani hapo kuhusiana na tukio alilolifanya, Breivik amesema kuwa hajutii kitendo hicho na alitarajia kuua watu wengi zaidi kuliko hata ilivyotarajiwa.

Mahakama pia imeitaka Polisi kuendelea na upelelezi wao dhidi ya mtuhumiwa huyo huku wakitaka kuchunguza watu wengine ambao huenda walishirikiana na Breivik kutekeleza mashambulizi hayo, hasa ikizingatiwa hata yeye mwenyewe amekiri kuwa na uhusiano na watu wengine katika kutekeleza mauaji hayo.

Breivik ambaye awali kabla ya kesi hiyo alitaka avalishwe mavazi ya kijeshi ndipo aingie mahakamani hapo, alikataliwa ombi lake na majaji na kuamuriwa kuvaa nguo za kawaida.

Polisi wamesema kuwa baada ya kumuhoji kwa masaa kadhaa mtuhumiwa huyo, amekiri kuhusika na mashambulizi yote na kuwa alilenga kuikosoa serikali na sera zake za mambo ya nje akisema wanasiasa wameishauri serikali vibaya na kukubali kutawaliwa na Uislamu.

Breivik aliwasili katika mahakama ya mjini Oslo chini ya ulinzi mkali wa polisi huku waandishi wa habari na watu wengine wakikataliwa kuhudhuria ndani wakati kesi hiyo ikiendelea kwa kile kilichoelezwa ni sababu za kiusalama.

Walati mtuhumiwa huyo akipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu, nchi hiyo hii leo ilisimama kwa dakika moja kukumbuka watu waliopoteza maisha ambapo maelfu ya wananchi waliweka mataji ya maua mjini Oslo na visiwa vya Utoya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.