Pata taarifa kuu
NORWAY

Anders Behring Breivik raia wa Norway akiri kuhusika na mashambulizi ya siku ya Ijumaa

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya mabomu na kushambulia kwa risasi yaliyotokea katika mji wa Oslo na kisiwa cha Utoya, Anders Breivik amekiri kuhusika na mashambulizi hayo.

Picha iliyotolewa na polisi ikimuonesha mtuhumiwa akitekeleza mauji
Picha iliyotolewa na polisi ikimuonesha mtuhumiwa akitekeleza mauji Norway Police
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria anayemtetea mtuhumiwa huyo amesema kuwa mteja wake amekiri kuhusika na mashmabulizi yote mawili ingawa hakuweza kuweka wazi lengo lake hasa la kutekeleza mashambulizi yayo yaliyoua watu 92.

Breivik alikamatwa na maofisa wa usalama muda mchache baada ya kuwashambulia kwa risasi vijana waliokuwa wamepiga kambi katika visiwa vya Utoya ambao aliwaua watu 85.

Polisi wanaendelea na msako wa watu wengine katika kisiwa cha Utoya ambapo hawafahamiki waliko hadi sasa.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na hukumu ya adhabu ya miaka 21 jela endapo akipatikana na hatia ya kutenda makosa hayo kwa mujibu wa sheria za ugaidi nchini humo.

Wakati huohuo amelfu ya wananchi wa Norway wameendelea kuomboleza msiba huo huku wakitaka serikali kuyashughulikia makundi yote ta mrengo wa kushoto amgayo yamekuwa yakipinga serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.