Pata taarifa kuu
Italia -IMF

Italia yatakiwa na IMF kuchukuwa hatuwa madhubuti za kubana matumizi

Shirika la Fedha duniani IMF limeitaka nchi ya Italia kuhakikisha inachukua hatua madhubuti za kubana matumizi ili kukabilina na mgogoro wa kifedha unaoinyemelea nchi hiyo.

Bodi ya uonbgozi wa IMF
Bodi ya uonbgozi wa IMF ©Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya IMF inakuja wakati mawaziri wa Umoja wa Ulaya wakifanya mkutano mjini Brussels kujadili hali ya kifedha barani humo, ambapo pamoja na mambo mengine wanajadili hali ya uchumi kwa nchi ya Italia ambayo huenda ikakumbwa na mgogoro wa kifedha isipochukua hatua za kubana matumizi.

Tayari waziri mkuu wa Italia Silvio Berluscone ametangaza hatua ambazo serikali yake itazichukua, hatua ambazo hata hivyo zimeonekana kupingwa na mawaziri hao wakihofia kutokea kama kile kilichoikumba nchi ya Ugiriki na kusababisha kuenea katika mataifa mengine.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.