Pata taarifa kuu
Yemen

Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh awahutubia wananchi kupitia luninga ya Yemen

Baada ya kushambuliwa na wananchi wanaotaka mabadiliko nchini Yemen, Rais Ali Abdullah Saleh, aliyekimbizwa Saudi Arabia kupatiwa matibabu, amewahutubia raia hao akiwa jijini Riyadh, akisisitiza kuwepo kwa mazungumzo ili kumalizavurugu za kisiasa nchini humo.

Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh akihutubia wananchi wa taifa lake kupitia Runinga ya Yemen Julay 7.7 2011.
Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh akihutubia wananchi wa taifa lake kupitia Runinga ya Yemen Julay 7.7 2011. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uso wake ukionesha makovu ya moto na mikono yake ikiwa imefunikwa na bendeji, Saleh alitoa hotuba hiyo kupitia luninga ya taifa.

Kiongozi huyo aliyefika jijini Riyadh, Saudi Arabia tangu tarehe 3 mwezi uliopita, alieleza jinsi alivyopatiwa matibabu na kubainisha kuwa amefanyiwa upasuaji mara nane, na madaktari wamefanikiwa kuondoa vipande vipande vya vyuma, vilivyoingia mwilini baada ya kufyatuliwa risasi na kupigwa mabomu.

Hatahivyo, Saleh ambaye ilikuwa vigumu kumtambua usoni hakuweka bayana iwapo ana mpango wa kuondoka madarakani.

Mtawala huyo mwenye umri wa miaka 69 alisema njia muafaka ya kumaliza tofauti zilizopo baina ya serikali na upizani ni kufanya mazungumzo, mbinu ya kidemokrasia, inayotambulika kikatiba na kisheria.

Aidha, Saleh anayetarajiwa kumaliza muhula wake mwaka 2013, amemshukuru makamu wake Abdrabuh Mansur Hadi, aliyekuwa akishinikizwa na jumuiya ya kimataifa na raia wa Yemen, kuchukua madaraka ya Rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.