Pata taarifa kuu
Libya

Waasi nchini Libya waendeleza mashambulizi licha ya mazungumzo ambayo yaendelea

Licha ya mazungumzo ya kusaka amani yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika na nchi ya Urusi kuhusu Libya yakiendelea waasi wa nchi hiyo wameendelea na mashambulizi zaidi dhidi ya vikosi vya serikali ambapo wamefanikiwa kumiliki mji wa al Qawalish.

ibtimes
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo ambayo yameelezwa kudumu kwa zaidi ya saa sita yamesaidia vikosi vya waasi kuyarejesha nyuma majeshi ya kanali Muamar Gaddafi ambayo yalikuwa yanaushikilia mji huo ulio jirani kuelekea mji wa Tripoli.

Wapiganaji hao wameacha kutumia magari yao kuingia mjini humo kuhofia mashambulizi ya kushtukiza ya vikosi vya serkali ambapo wamekuwa wakiendesha msako wa nyumba kwa nyumba kujiridhisha kama wanajeshi wa Gaddafi wameondoka.

Msemaji wa waasi anayeongoza mapambano hayo amesema kuwa kushikilia mji huo ni mafanikio ambayo yatawarahisishia njia ya kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli ambao ndio shabaha yao kwa sasa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.