Pata taarifa kuu
Syria

Amnesty International yaishutumu serikali ya Syria kukiuka haki za binadamu

Shirika la kimatiafa linalotetea haki za binadamu duniani la Amnesty International limetoa ripoti yake inayoonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya serikali ya Syria. 

Wananchi wa Syria wakiandamana
Wananchi wa Syria wakiandamana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo lenye makazi yake nchini Uingereza limeituhumu vikali serikali ya Syria kufuatia mauaji ya raia yanayoendelea kufanywa na vikosi vyake bila kujali miito ya jumuiya ya kimataifa kutaka kusitishwa kwa mauaji hayo.

Ripoti hiyo imelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhakikisha linachukua hatua za haraka dhidi ya serikali ya nchi hiyo kwa lengo la kusitisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya nchi hiyo.

Shirika hilo limesema kuwa limewahoji wananchi na wanaharakati zaidi ya 50 ambao wote wamekiri kuwa vikosi vya serikali vimekuwa vikiua raia wasio na hatia.

Ripoti hiyo inaongeza shinikizo zaidi kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad na utawala wake kusitisha machafuko yanayoendelea nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.