Pata taarifa kuu
Pakistani-Afghanistani

Pakistani na Afghanistani kushirikiana kudumisha amani

Viongozi wa Pakistani na Afghanistan wameapa kupambana na ugaidi na kupanua ushirikiano wao ili kusaidia kuleta amani katika maeneo hayo. Mazungumzo yaliyofanyika na rais wa Afghanistan Hamid Karzai na wa Pakistan Asif Ali Zardari yamelenga kuweka juhudi kuwa na mazungumzo ya amani na makundi ya Taliban.

Askari wa kimataifa nchini Afghanistani
Askari wa kimataifa nchini Afghanistani REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Karzai nchini Afghanistan imekuja ikiwa ni wiki kadhaa baada kuuawa kwa Kiongozi wa makundi ya kigaidi Osama Bin Laden mjini Abotabad nchini Pakistani..huku kukiwekwa shinikizo na marekani kuwepo na mazungumzo ya amani nchini humo ambayo yatawezesha vikosi vya marekani kuondoka nchini humo.

Nae rais wa zamani Burhanuddin Rabbani anayehodhi baraza la amani nchini Afghanistan ameiomba pakistan kusaidia kumaliza mgogoro nchini Afghanistan baada ya kuwa na mazungumzo na kiongozi wa chama kimoja maarufu cha kiislam anayeunga mkono taliban Fazla Rehman,ambaye amesema anaunga mkono jitihada za mazungumzo na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa unaofanywa na wadau hao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.