Pata taarifa kuu
PAKISTAN-PENSHAWAR

Watu 35 wamekufa katika milipuko miwili mjini Penshawar, Pakistan

Watu zaidi ya 35 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa nchini Pakistan baada ya kutokea mlipuko katika soko moja kwenye mji wa Penshawar.

Polisi nchini Pkistan wakifanya ukaguzi katika eneo la Penshawar ambako kumetokea milipuko miwili
Polisi nchini Pkistan wakifanya ukaguzi katika eneo la Penshawar ambako kumetokea milipuko miwili REUTERS/Fayaz Aziz
Matangazo ya kibiashara

Polisi katika mji wa Penshawar wamesema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha milipuko hiyo ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa milipuko hiyo ilikuwa ni mabomu ya kutegwa.

Kamanda wa kikosi maalumu cha upelelezi kilichoelekea katika eneo la tukio Dost Mohhamed amesema kuwa mlipuko wa kwanza ulikuwa mdogo ambapo baadae kulitokea mlipuko mkubwa na kusababisha vifo hivyo vya watu 15 na kujeruhi wengine zaidi ya 40.

Wakati huohuo ameongeza kuwa katika operesheni ambayo majeshi ya Pakistan imeyafanya katika mji wa Makeen jirani na mpaka wake na nchi ya Afghanistan wamefanikiwa kuwaua wapiganaji kadhaa wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa Taliban.

Kufuatia shambulio hilo serikali ya Pakistan imewashutumu vikali wapiganaji wa Taliban nchini humo kwa kuendeleza mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia katika kutekeleza vitendo vyao vya ugaidi.

Tangu kuuawa kwa kiongozi wa kundi la al Qaeda dunini nchini humo Osama Bin Laden, mashambulizi toka kwa wapiganaji wa kundi hilo na wale wa Taliban wamekuwa wakiongeza mshambulizi dhidi ya raia na wanajeshi wa Pakistan kwa lengo la kulipiza kisasi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.