Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Clinton: Afrika pigeni vita ukoloni mambo leo

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton ameendelea na ziara yake katika bara la afrika ziara ambayo atatembelea mataifa matatu ya afrika, jana alikuwa mjini Lusaka zambia kufunga mkutano wa uchumi uliofanyika nchini Zambia nakuwataka viongozi hao kushirikiana na nchi yake katika biashara.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ni ziara ya kwanza kwa waziri huyo kuifanya katika mataifa ya kusini mwa Afrika kwa mwaka huu, amabpo siku ya ijumaa alifungua mkutano wa biashara uliowakutanisha mawaziri toka mataifa mbalimbali ya Afrika, mkutano uliozungumzia uhusiano wa kibiashara na mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani.

Hii leo waziri Clinto alianza ziara rasmi nchini Zambia kwa kufungua kituo cha biashara kati ya nchi yake na Zambia na kuahidi kuisaidia nchi hiyo katika biashara na kukuza uchumi wa taifa hilo huku akipongeza juhudi za rais wa nchi hiyo Rupiah Banda kwa juhudi zake za kukuza uchumi wa taifa hilo.

Akizungumzia malengo ya kufunguliwa kwa kituo hicho, wazir clinto amesema kwa kitasaidia kukuza biashra za ndani na biashara za kimataifa ikiwemo nchi yake na kuwa hata nchi za Jirani zitanufaika na kituo hicho.

Akizungumza kwa nyakati tofauti, waziri Clinton amesifu juhudi za mataifa ya Afrika katika kufanya biashara na mataifa ya Ualaya ingawa kuna hofu ya kuenea kwa ukoloni mambo leo katika bara hilo.

Waziri huyo pia amekosoa nchi za Afrika kukubali kujiingiza katika biashara na nchi ya China na kuruhusu uwekezaji mkubwa wa taifa hilo barani Afrika na kujikuta nchi nyingi zikipata hasara katika baadhi ya meneo kutokana na kukosa ubora wa soko la China.

Nchi ya China ni moja kati ya mataifa yaliyokuja juu kiuchumi ambapo sasa inashikilia nafasi ya Pili nyuma ya Marekani na ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na uwekezaji mkubwa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.