Pata taarifa kuu
PAKISTAN-AFGHANISTAN

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ziarani nchini Pakistan

Raisi wa Afghanistan Hamid Karzai leo amesafiri kuelekea nchini Pakistan kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kukutana na rais Asif Ali Zardari na waziri mkuu Yousuf Raza Gilan.

Raisi wa Afghanistan Hamid Karzaï ambaye hii leo amesafiri kuelekea nchini Pakistan
Raisi wa Afghanistan Hamid Karzaï ambaye hii leo amesafiri kuelekea nchini Pakistan Reuters / Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kufanywa na kiogozi huyo tangu makomandoo wa Marekani wafanikiwe kumuua kiongozi wa Al-Qaeda nchini humo Osama Bin Laden ziara inayotarajia kujadili hali ya usalama katika mipaka ya nchi hizo mbili.

Wachambuzi wa masuala ya mambo wanasema kuwa zaira hiyo pia inalenga kuimarisha uhusiano kati ya serikali ya Kabul na Islamabad ambazo kwa pamoja zimekuwa zikipigana na wanamgambo wa Taliban nchini mwao.

Rais Karzai ameambatana na ujumbe wa maofisa 50 wa serikali yake ambapo watakutana na viongozi wa Pakistan kwa nyakati tofauti kujadili mustakabali wa hali ya usalama kati ya nchi hizo mbili.

Kubwa ambalo linatarajiwa kujadiliwa katika ziara hiyo ni kuhusiana na operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Taliban, operesheni ambayo nchi ya Pakistan, Afghanistan na Marekani wamekuwa wakishirikiana katika kufanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Taliban.

Wakati rais Karzai akifanya ziara hiyo tayari kumezuka hofu ya wanamgambi wa Taliban kufanya mashambulizi wakati wa ziara hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.