Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUD ARABIA

Serikali ya Yemen yakataa kufanya mazungumzo na upinzani

Serikali ya Yemen imekataa ombi la muungano wa vyama vya upinzani JMP, lenye nia ya kufanya mazungumzo juu ya mabadiliko ya mpito ya kisiasa nchini humo.

Wapiganaji watiif wa cheikh Sadeq al-Ahmar
Wapiganaji watiif wa cheikh Sadeq al-Ahmar REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mmoja wa juu ambaye hakutaka kutaja jina lake, amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoweza kufanywa baina ya pande hizo, mpaka Rais Ali Abdullah Saleh, arejee kutoka Saudi Arabia, anakopatiwa matibabu.

Kauli hiyo imepokewa kwa ghadhabu, na kufuatiwa na maelfu ya wananchi kuandamana mbele ya makazi ya Abdu-Rabbu Mansour, makamu wa rais wa Yemen, wakimshinikiza kiongozi huyo kuunda baraza la mpito.

Maelfu ya wananchi walisikika wakiimba nyimbo za mapinduzi huku wakiwa wamebeba mabango yanayokashifu utawala wa Rais Saleh huku wakiendelea kushinikiza kuundwa mapema kwa serikali ya mpito kabla ya rais huyo ahajrejea nchini akitokea Saud Arabia.

Upinzani nchini humo umekuwa ukishinikiza kufanyika kwa mazungumzo hivi sasa ambapo awali mara baada ya kutolewa kwa taarifa za kupelekwa nje ya nchi kwa Rais Saleh waliunga mkono uteuzi wa makamu wa rais Abdu-Rabbu Mansour ambaye anatokeo kusini mwa nchi hiyo ambako ndiko maandamano yalipoanzia.

Maofisa kadhaa wa serikali ya Yemen wameendelea kusisitiza kuwa rais Saleh ataendelea kuwa kiongozi halali wa nchi hiyo mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo ama kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.

Taarifa kutoka nchini Saud Arabia zinasema kuwa rais Saleh ameendelea kupatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio la juma lililopita ambapo amefanyiwa upasuaji katika kifua.

Hata hivyo inaelezwa kuwa hali ya kiongozi huyo imeendelea kudhoofu kinyume na awali ilivyoelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri kitu kinachoashiria kuwa huenda kiongozi huyo asirejee nchini mwake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.