Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUD ARABIA

Rais wa Yemen apelekwa nchini Saudi Arabia kwa matibabu zaidi

Rais wa Yemen Ali abdulah Saleh amehamishiwa nchini Saud Arabia kwa matibabu zaidi kufuatia kujeruhiwa katika shambulio la ijumaa kwenye makazi yake wakati akisali.

Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh
Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mji wa sanaa ulilipuka kwa shamrashamra kufuatia taarifa ya serikali kudhibitisha kuwa kiongozi huyo amepelekwa nchini saudi arabia kwa matibabu huku akimwachia majukumu ya kukaimu kiti hicho makamu wake wa rais.

Hata hivyo chama tawala nchini humo bado hakijaamua kumtangaza rasmi makamu huyo wa rais kuchukua rasmi madaraka ya kukaimu uongozi wa nchi hiyo wakati huu ambapo rais Saleh hayupo wakihofia kiongozi huyo kushirikiana na upinzani.

Abdel Rabbo Mansur Hadi kiongozi ambaye anatarajiwa kushika madaraka ya urais kwa muda anatoka kusini mwa nchi hiyo, eneo ambalo ndiko upinzani unanguvu kubwa kitu kinachowatia hofu maofisa wa chama tawala kuamua kumtangaza rasmi.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni ushindi kwa upinzani, viongozi wengi wa kambi ya uoinzani wameonekana kukubaliana na uteuzi wa bwana Abdel Rabbo Mansur Hadi kushika wadhifa wa urais kwa muda wakiamini kuwa huenda kiongozi huyo kwakuwa anatoka kusini mwa nchi hiyo akasikiliza madai yao akisimikwa rasmi kushika wadhifa huo.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema kuwa huenda kuondoka kwa rais saleh kukachochea vurugu zaidi nchini humo huku wakieleza kuwa upo uwezekano wa rais huyo kutorejea nchini mwake.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo endapo kiongozi huyo hatarejea nchini mwake ndai ya siku tisini basi makamu wake wa rais atashika rasmi madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.