Pata taarifa kuu
PAKISTAN-WAZIRISTAN

Wanajeshi wa Pakistan wajiandaa kufanya mashambulizi katika jimbo la Waziristan

Taarifa kutoka mjini Islamabad nchini Pakistan zinasema kuwa maofisa wa juu wa jeshi la nchi hiyo walikutana juma lililopita na kukubaliana kupanga mashambulizi dhidi ya kundi la mtandao wa Haqqani lenye makao yake mpakani mwa nchi hiyo na Afghanistan kaskazini mwa jimbo la Waziristan.

Askari wa Pakistan wakiwa katika doria jimboni Waziristan
Askari wa Pakistan wakiwa katika doria jimboni Waziristan ©Reuters/ Faisal Mahmood
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa ubalozi wa marekani nchini humo wamenukuliwa na vyombo wakisema kuwa wamesikia uwepo wa taarifa hizo lakini wanaendelea kuwasiliana na viongozi wa juu wa jeshi la Pakistan kudhibitisha ukweli huo.

Maofisa usalama wa Pakistna mjini Islamabad walipoulizwa kuhusiana na operesheni hiyo hawakuweza kuzungumzia chochote zaidi ya kukiri kuwa watu wa usalama walikutana juma lililopita kuzungumzia hali ya mambo katika jimbo la Waziristan kaskazini mwa nchi hiyo na mpaka na Afghanistan.

Kundi la mtandao wa Haqqani limekuwa likiendesha mashambulizi dhidi ya rais kutokea mpakani mwa nchi hiyo na Afghanistan katika jimbo la Waziristan ambapo juma hili wanajeshi kadhaa waliripotiwa kuuawa na wapiganaji wa kundi hilo.

Mbali na kundi hilo lenye makazi yake katika jimbo hilo pia wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Taliban nao wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Pakistan na vile vya Marekani wakitokea mpakani mwa nchi ya Afghanistan.

Operesheni hiyo inatarajiwa kuwa ya mashambulizi ya ardhini na angani, operesheni inayotarajiwa pia kuvishirikisha vikosi vya Marekani vilivyoko nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.