Pata taarifa kuu
YEMEN

Wapiganaji wa Al Qaeda nchini Yemen wauteka mji wa Abyan

Wapiganaji wa mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda walioko nchini Yemen wametangaza kuuteka mji wa Abyan na kuahidi kuendelea kuiteka miji zaidi.

Umati wa wananchi wa Yemen wakiandamana kupinga serikali
Umati wa wananchi wa Yemen wakiandamana kupinga serikali REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao walioitoa leo viongozi wa kundi hilo wamesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuteka eneo la Zinjibar lililoko kusini mwa mji wa Abyan na kuahidi kuendelea kuteka miji zaidi.

Hatua ya kundi hilo kuteka mji huo inakuja wakati ambapo nchi hiyo imeingia katika machafuko ambapo raia wakiongozwa na viongozi wa makabila wameanzisha mapambano dhidi ya polisi na kuteka baadhi ya majengo ya ofisi za serikali.

Mpaka sasa zaidi ya watu 120 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mapigano hayo katika miji ya kusini mwa nchi hiyo ambapo maelfu ya watu wanakimbilia mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa ambako kuna ulinzi mkali wa vikosi vya serikali.

Wakati machafuko hayo yakiendelea bado rais Ali Abdulah Salleh ameendelea kusisitiza msimamo wake wakutoachia madaraka na kusababisha kuendelea kutokea kwa machafuko toka kwa waandamanaji wanaoipinga serikali ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.