Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI

Uturuki wakataa uharakishaji wa kumuondoa madarakani Rais wa Syria Bashar Al Assad

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema ni mapema kuamua iwapo Rais wa Syria Bashar Al Assad aondoke madarakani na badala yake inabidi juhudi ziongezwe kudhibiti machafuko yanayoendelea kuchangia vifo vya mamia ya wananchi.

Waandamanaji nchini Syria wakiwa wamejitokeza katika Jiji la Banias
Waandamanaji nchini Syria wakiwa wamejitokeza katika Jiji la Banias REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Erdogan amekiri Rais Assad ni rafiki yake wa karibu lakini nchi yake imeanza kufanya mabadiliko ya utawala kabla hata ya wimbi la mabadiliko katika nchi za Kiarabu halijaanza.

Erdogan amesema Kiongozi huyo wa Syria ambaye anapendwa na wananchi wake anachukua hatua za kumaliza mtafuruku uliopo ambapo kwa sasa juhudi za kuleta mabadiliko zimeanza kuonekana.

Kwenye mahojiano na Kituo Kimoja cha Televisheni nchini Marekani Waziri Mkuu Erdogan alipouulizwa kama huu wakati wa Rais Assad kuondoka alikana na kuanisha ni mapema mno kufanya hivyo.

Erdogan ameongeza kuwa mwaka jana alifanya mazungumzo ya muda mrefu na Rais Assad wakijadili kuondoa hali ya hatari, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi pamoja na kuruhusu vyama vingi.

Kauli hii ya kuzuia shinikizo la kumuonda madarakani Rais Assad linakuja wakati ambapo wanajeshi wa Syria wakimuaa mwandamanaji mmoja ambaye ni Mwanaharakati Nawar Al Omar.

Wanajeshi wakitumia risasi za moto pamoja na vifaru wamewatawanya maelfu ya Wanaharakati ambao wameitisha maandamano kuongeza shinikizo la kufanyika mabadiliko nchini Syria.

Kusini mwa Mji wa Daraa wanajeshi walifyatua risasi kuwatisha wandamanaji ili waweze kusambaratika baada ya kuitisha maandamano kupinga Utawala wa Rais Assad.

Wanaharakati wakiwahamasisha wananchi waliingia kwenye mitaa mbalimbali nchini Syria baada ya kumalizika kwa Ibada ya Ijumaa kitu ambacho kiliwachukiza wanajeshi na hivyo kuzima maandamano hayo kwa kutumia nguvu kubwa.

Katika hatua nyingine majeshi ya nchi hiyo yameanza kuondolewa katika Mkoa wa Pwani wa Banias ambapo walikuwa wanashika doria Waziri wa Habari Adnan Mahmud amewaambia wanahabari.

Waziri wa Habari Mahmud amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuimarika kwa ulinzi katika Jimbo hilo la Banias kitu ambacho kinawasukuma kuchukua uamuzi wa kuondoa majeshi.

Tangu kuanza kwa maandamano nchini Syria takwimu zinaonesha kuwa watu wanaokadiriwa kufikia 850 wamepoteza maisha katika Majiji ya Daraa, Homs na Banias.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.