Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Waziri Pakistani akiri kupewa taarifa za Operesheni ya kumuua Osama Bin Laden baada ya kuanza

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistani Rehman Malik amekiri kufahamu operesheni ya Makomandoo wa Marekani dakika kumi na tano baada ya kuanza mpango huo wa kumuua Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Osama Bin Laden juma moja lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ametoa kauli hiyo wakati wa Mahojiano maaluma ambayo amefanya na Kituo Cha Televisheni cha Al Arabiya na kuthibitisha kupewa taarifa za operesheni hiyo.

Malik ametoa tamko hilo huku akisema nia yake ni kutaka kuona ushirikiano madhubuti kati ya Islamabad na Washington ili kuweza kufanikisha vita dhidi ya ugaidi.

Helkopta yenye Makomandoo wa Marekani ilifanikisha kifo cha Osama Bin Laden tarehe 2 ya Mwezi Mei baada ya kuvamia nyumba aliyokuwa anaishi jirani na Kambi ya Jeshi ya Pakistan na kisha kuuzika mwili wake baharini.

Kauli hii ya Waziri Malik inakuja wakati ambapo Rais wa Marekani Barack Hussein Obama ameitaka Pakistani kuanza kufanya uchunguzi kubaini ni kwa namna gani Osama alifanikiwa kuishi kwa miaka kadhaa karibu na Kambi ya Jeshi.

Rais Obama amesema kumekuwa na mawazo kuwa Osama Bin Laden ana mtandao madhubuti ambao umefanikisha yeye akaishi kwa miaka kadhaa nchini Pakistani bila ya kufahamika iwepo wake.

00:31

President Barack Obama Urges Pakistan to Probe Osama Resident

Kiongozi huyo wa Marekani licha ya kuanisha hatua yake ya kuamini uwepo wa mtandao huo lakini hawajui kina nani wanasaidia mtandao huo wa Al Qaeda na je watu hao wanatoka serikali au sehemu gani?
Kwa upande wake Ikulu ya Marekani “White House” imeendelea kuomba msaada wa ushirikiano kutoka Pakistani ili waweze kuwapata wake watatu wa Osama Bin Laden ambao wanaamini watakuwa na maelezo ya kutosha juu ya Mtandao wa Al Qaeda.

Wake hao wa Osama Bin Laden kwa sasa wapo kizuizini nchini Pakistani wakati huu ambapo uchunguzi mkali unaendelea kubaini taarifa za siri za Mtandao wa Al Qaeda.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani anatarajiwa kutoa taarifa fupi Bungeni juu ya operesheni ya Marekani ambayo imefanikisha kifo cha Osama Bin Laden juma moja lililopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.