Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Montenegro: Uchaguzi ambao unaweza kuashiria mabadiliko katika historia ya nchi

Wapiga kura nchini Montenegro wanaitwa kupiga kura Jumapili hii, Machi 19 kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. Kura ambayo inaweza kuashiria mabadiliko katika historia ya nchi hiyo ndogo, inayokumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa miezi kadhaa.

Bango la kampeni ya Milo Djukanovic, huko Podgorica, Machi 16, 2023.
Bango la kampeni ya Milo Djukanovic, huko Podgorica, Machi 16, 2023. AP - Risto Bozovic
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mmoja, kuna mkongwe wa siasa za Balkan, Milo Djukanovic, ambaye amebadilishana kwa miaka 32 kati ya majukumu ya Waziri Mkuu na Rais wa Jamhuri, lakini ambaye haanzii kama mtu anayependelea kupata mamlaka mpya katika uongozi wa nchi, kwa sababu amepoteza imani tangu Chama chake cha Kidemokrasia cha Soshalisti kukataliwa na wapiga kura katika uchaguzi wa wabunge wa mwezi Agosti 2020.

Anakabiliwa na wagombea kadhaa kutoka kwa kundi jipya la wengi , ambalo hujumuisha wanasiasa wanaopigana na sera zake. Milo Djukanovic ana "mshindani wake anayepewa nafasi zaidi", ambaye ni kiongozi wa chama cha Democratic Front, anayeunga mkono Serbia na Urusi. rais anayemaliea muda wake anataka kujionyesha kama mdhamini pekee wa ahadi za Ulaya na kiongozi wa Montenegro anayeunga mkono nchi za Magharibi.

Hata hivyo, hoja zake hazizingatiwi tena na umma, na ni mwanauchumi Jakov Milatovic ambaye anapewa nafasi ya kushinda duru ya pili. Hakika, raia wamechoshwa na ugomvi wa utambulisho na hotuba za kizalendo; badala yake, raia wanatarajia kuboreshwa kwa hali yao ya maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.