Pata taarifa kuu

China: Rais Xi Jinping kuimarisha zaidi usalama wa taifa lake

NAIROBI – Rais wa China Xi Jinping amesisitiza haja ya kuimarisha usalama wa kitaifa, katika hotuba yake ya kwanza tangu ateuliwe kuhudumu kwa muhula wa tatu kama rais wa nchi hiyo.

Rais wa China Xi Jiping
Rais wa China Xi Jiping AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Rais Xi amewaambia wajumbe waliokusanyika katika kikao cha kufunga mkutano wa chama cha The National People's Congress NPC kuwa usalama ni msingi wa maendeleo lakini pia utulivu ni sharti la ustawi.

Katika hotuba yake, Xi amewashukuru maelfu ya wajumbe kwa kumpa nafasi ya kuhudumu kwa muhula wa tatu, huku akiahidi kushughulikia mahitaji ya nchi na maslahi ya wananchi.

Aidha ametoa wito wa kuimarishwa kwa utulivu katika mji wa Hong Kong na kisiwa kinachojitawala cha Taiwan, ambacho China inakiona kama sehemu ya himaya yake.

Juma lililopita, bunge lilimuidhinishwa xi kuhudumu kama rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka metano, na kumafanya kuwa kiongozi mwenye ushawishi zaidi katika historia ya nchi hiyo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.