Pata taarifa kuu
MYANMAR- SIASA.

Myanmar: Jeshi limewanyonga wanaharakati 4 wa demokraisa

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umewanyonga wanaharakati wanne wa demokraisa katika kile ambacho kimetajwa kuwa mwanzo wa kutumika kwa hukumu ya kunyongwa nchini humo baada ya miaka mingi.

Mbunge wa zamani nchini Myanmar ,Phyo Zeya Thaw akiwa na  Aung San Suu Kyi
Mbunge wa zamani nchini Myanmar ,Phyo Zeya Thaw akiwa na Aung San Suu Kyi © AP
Matangazo ya kibiashara

Wanne hao akiwemo mbunge wa zamani Phyo Zeya Thaw, mwandishi wa vitabu na mwanaharakati Ko Jimmy, Hla Myo Aung pamoja na Aung Thura Zaw walituhumiwa kwa kutekeleza makosa ya ugaidi.

Jeshi nchini humo mwezi Juni lilitangaza kuanza kutekeleza hukumu hiyo hatua iliokashifiwa vikali kimataifa.Hukumu hiyo inakuja baada ya jeshi kuchukua madaraka mwaka wa 2021.

Jeshi lilichukua madaraka kutoka kwa serikali ya kiraia chini ya uwongozi wa Aung San Suu Kyi hali iliyosababisha mandamano makubwa ya raia mwezi Feburuari mwaka jana, waandamanaji wakikabiliwa kwa nguvu na wanajeshi.

Umoja wa mataifa umesema hukumu hiyo ya kunyongwa ni ya kwanza nchini humo tangu mwaka wa 1988.

Hukumu ya kunyongwa kwa wanne hao iliaafikiwa mwezi Januari, mashirika ya kutetea haki za bindamu yakikashifu hukumu hiyo iliotajwa kutokuwa na uwazi.

Phyo Zeya Tha na Kyaw Min Yu, walipata pigo mwezi Juni baada ya ombi la kutaka kubatilishwa kwa hukumu dhidi yao kutupiliwa mbali.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres alikuwa ametaja hukumu ya kifo dhidi ya wanne hao kuwa ukiukaji wa haki ya kuishi, uhuru na usalama wa binadamu.

Uwongozi wa kijeshi nchini humo umetuhumiwa kwa kuwakamata wanaharakati na wapinzani wanaopinga hatua yake ya kuchukua madaraka mwaka jana.

Jeshi lilipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliokipa ushindi mkubwa chama cha Suu Kyi, jeshi likisema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udaganyifu –Madai ambayo maofisa wa tume ya uchaguzi walikana wakisema hakuwepo na ushahidi ya kudhibitisha uwepo wa udaganyifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.