Pata taarifa kuu

India: Wazazi wamshtaki mwanao wa kiume kwa kuchelewa kuwapa mjuku

Wanadoa wawili kaskazini mwa India katika jimbo la Uttarakhand, wamefunguliwa kesi mwanao wa kiume pamoja na mkewe kwa kukosa kuwapa wajuku hata baada yao kuwa katika ndoa kwa kipindi cha miaka 6.

Wanandoa nchini India
Wanandoa nchini India DR
Matangazo ya kibiashara

Sanjeev na Sadhana Prasad, wenye umri wa miaka 61 na 57, wanasema kuwa walitumia akiba yao kumlea kijana wao ambapo pia walimlipia karo katika taasisi ya kusomea urubani na kisha baadae wakadhamini harusi yake ya kifaraha iliyofana zaidi.

Wazazi hao kwa sasa wanadai kurejeshwa karibia dolla za marekani milioni 650,000 iwapo mwanao wa kiume hatapata mtoto katika kipindi cha mwaka moja.

Sadhana Prasad, ameeleza kuwa amefungua kesi hiyo dhidi ya mwanao kwa vile swala la gharama walioitumia kumsomesha linamtatiza kiakili, Kesi ambayo kijana wao haijaizungumzia.

Kwa mujibu wa wazazi hao, mwanao wa kiume Shrey Sagar, alirejee nchini India mwaka wa 2007 baada ya kupoteza ajira yake hali iliyowalazimu kushugulikia mahitaji yake ya kifedha kwa zaidi ya kipindi cha miaka miwili.

Babake Shrey Sagar, 35, anaeleza kuwa iwapo kijana wake atapata mtoto atakuwa amemaliza machungu walio nayo kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.