Pata taarifa kuu

Ghadhabu nchini India baada ya mlemavu kuzuiwa kuabiri ndege.

Serikali nchini India, imesema imeanza kuichunguza kampuni moja ya ndege inayotoa huduma za usafiri wa anga kwa abiria wanaosafiri ndani mwa taifa hilo kufuatia kuwepo kwa madai kuwa kampuni hiyo ilimzuia kijana mlemavu kuabiri ndege ya kampuni hiyo.

Ndege za kampuni ya IndiGo ya nchini India.
Ndege za kampuni ya IndiGo ya nchini India. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaeleza kuwa muhudumu wa kampuni hiyo ya ndege aliwaeleza wazazi wa kijana huyo kwamba uwepo wake kwenye ndege hiyo ungehatarisha wasafiri wengine.

Tukio hili limezua hisia mseto kote duniani baadhi wakitaja kitendo hicho kama cha kibaguzi, madai ambayo kampuni ya IndiGo inayomiliki ndege hiyo  imekana ikisema  inajivunia kutoa huduma zake kwa kila mtu.

Waziri wa katika wizara wa mambo ya usafiri wa anga nchini humo Jyotiraditya Scindia, amesema kuwa anafuatilia tukio hilo kwa ukaribu na iwapo kampuni hiyo itapatikana na kosa itachukuliwa hatua za kisheria.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika uwanja wa ndege wa Ranchi, siku ya jumamosi ya wiki jana, limetambulishwa kwa umma baada ya Manisha Gupta abiria aliyekuwa anasafiri pamoja na mwathiriwa kuchapisha katika ukurasa wake wa facebook.

Manisha, aidha anaeleza kuwa abiria wengine kwa ndege hiyo walijaribu kuwashawishi wahudumu hao wa ndege kumuruhusu kijana huyo kuabiri ila hawakuitikia.

India ina zaidi ya watu milioni 26 wanaoishi na changamoto za kimaumbili ambao wanakumbwa na changamoto za usafiri kutokana na kutokuwepo kwa miundo mbinu inayojali mahitaji yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.