Pata taarifa kuu

Mzozo wa Ukraine: Xi Jinping na Vladimir Putin waonyesha ushirikiano wao wa karibu

Mazungumzo haya ya kwanza ya kidiplomasia baada ya takriban miaka miwili yanakuja katika muktadha wa mvutano uliokithiri kati ya Urusi na nchi za Magharibi kuhusu mzozo wa Ukraine, na kususiwa kwa michezo hii ya Olimpiki na wanasiasa wengi wa Magharibi.

Rais wa Urusi na mwenzake wa China mjini Beijing, Februari 4, 2022.
Rais wa Urusi na mwenzake wa China mjini Beijing, Februari 4, 2022. AP - Alexei Druzhinin
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin na Xi Jinping wakiwa bega kwa bega saa chache kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing. Bila shaka hii ndiyo taswira kali ya siku hiyo nchini China. Kama ilivyokuwa mwaka wa 2014, kwenye Michezo ya Olimpiki ya Sochi, Xi Jinping na Vladimir Putin wamekukaa mbele kuhudhuria sherehe ya kuzindua moja ya hafla za michezo zinazotangazwa zaidi kwenye sayari.

Urafiki wa kweli

Saa chache mapema wawili hao, wakionyesha tabasamu mbele ya kamera, bila kuvaa barakoa na wakikaribiana, walitaka kuonyesha urafiki usio na kikomo na uhusiano bora "usio na kifani". Tangu mwaka wa 2013, mwaka alipoingia madarakani, Xi Jinping amekutana na Vladimir Putin zaidi ya mara 30. Tukio la nadra katika uhusiano wa kimataifa.

Mkutano huu wa marais wa Urusi na China unakuja katika hali ya mvutano kati ya nchi za Magharibi kuhusiana na Ukraine na kususiwa kidiplomasia kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, kwa mpango wa Marekani. Washirika hao wawili walikuwa hawajaonana ana kwa ana tangu kuzuka  kwa janga la Covid-19. Na mkutano huu ulikuwa, kulingana na Xi Jinping, wa kwanza kwake na kiongozi wa kigeni kwa karibu miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.