Pata taarifa kuu
CHINA

Xi Jinping aataka usawa katika mfumo wa utawala duniani

Rais Xi Jinping wa China ametangaza leo Jumanne kwamba mfumo wa utawala wa dunia lazima ufanywe kwa usawa na uadilifu, huku akiongeza kuwa sheria zinazowekwa na nchi moja au zaidi haziwezi klazimishwa kutekelezwa na nchi zingine.

Rais wa China Xi Jinping akifungua mkutano wa Boao kwa Asia, huko Boao, mkoa wa Hainan, China Aprili 20, 2021.
Rais wa China Xi Jinping akifungua mkutano wa Boao kwa Asia, huko Boao, mkoa wa Hainan, China Aprili 20, 2021. REUTERS - Kevin Yao
Matangazo ya kibiashara

Akiongea katika Mkutano wa kila mwaka wa Boao kwa Asia, uliyoanzishwa na China kuiga Mkutano wa Davos, Xi Jinping amesema kuwekwa kwa vizuizi hakutanufaisha mtu yeyote.

Beijing kwa muda mrefu imekuwa ikitaka marekebisho katika taasisi za kimataifa ili maono ya nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na China, yaweze kuzingatiwa na sio tu zile zenye idadi ndogo ya raia kutoka nchi zenye nguvu.

"Ulimwengu unataka uadilifu, sio uhasama," amesema rais wa China. "Nchi kubwa lazima ionyeshe kuwa ni nchi nzuri kwa kuchukua majukumu zaidi," ameongeza, bila kutaja nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.