Pata taarifa kuu
BURMA

Burma yasherehekea "siku ya majeshi", maandamano yakandamizwa vikali

Jeshi la Burma llimefanya guaride kubwa katika kusherehekea "siku ya majeshi", iliyoandaliewa katika mji mkuu wa Naypyidaw Jumamosi hii Machi 27.

Wageni wanaangalia gwaride la kijeshi la Machi 27, Siku ya majeshi, katika mji mkuu wa Burma.
Wageni wanaangalia gwaride la kijeshi la Machi 27, Siku ya majeshi, katika mji mkuu wa Burma. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Miji kadhaa nchini humo imekumbwa na maandamano mapya ya wanaharakati wa demokrasia, maandamano ambayo yamekandamizwa na vikosi vya usalama vikishirkiana na vikosi vya ulinzi.

Maelfu ya askari walishiriki katika maandamano hayo, huku  kukifanyika maonyesho makubwa ya mizinga, makombora na helikopta za jeshi.

Katika mji mkuu wa nchi hiyo maafisa wakuu wa jeshi na maafisa wa ngazi za juu jeshi walikutana, mkutano ambao ulihudhuriwa na wajumbe kutoka  Urusi na China.

Kila mwaka katika tarehe hii, Tatmadaw, jina la jeshi la Burma, huandaa kwa "siku ya vikosi vya jeshi" gwaride kubwa la jeshi huko Naypyidaw, mbele ya afisa wake mkuu, ambaye kwa sasa kiongozi mkuu utawala wa kijeshi uliofanya mapinduzi: Jenerali Min Aung Hlaing. Lakini wakati huu, Burma inapitia mgogoro mkubwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1. Jumamosi hii, maandamano kadhaa yamekandamizwa vibaya na zaidi ya waandamanaji kumi wameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.