Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA-SIASA

Burma: Waandamanaji waingia tena mitaani licha ya ukandamizaji wa umwagaji damu

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia nchini Burma wamejitokeza tena mitaani leo Alhamisi kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, siku moja baada ya kushuhudiwa umwagaji damu zaidi tangu maandamano yalipoanza, ambapo watu 38 waliuawa kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Myanmar imeshuhudia ghasia na maandamano tangu Februari 1 baada ya jeshi kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi.
Myanmar imeshuhudia ghasia na maandamano tangu Februari 1 baada ya jeshi kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na waandishi wa habari wa nchini humo, maafisa wa polisi wamefyatua risasi Alhamisi hii asubuhi kutawanya waandamanaji huko Pathein, mji ulio magharibi mwa Rangoon. Hakuna visa vya majeruhi ambavyo vimeripotiwa mara moja.

Wanaharakati wanasema hawataki kuishi chini ya utawala wa kijeshi na wameamua kuendelea kushinikiza kuachiliwa kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aung San Suu Kyi na kutambuliwa kwa ushindi wa chama chake wakati wa uchaguzi wa wabunge wa mwezi Novemba mwaka jana.

"Tunajua tunaweza kupigwa risasi na kuuawa, lakini hakuna maana ya kuishi chini ya utawala wa kijeshi," Maung Saungkha, mmoja wa wanaharakati hao ameliambia shirika la habari la REUTERS.

Katika mji wa Yangon, jiji kuu la Burma, waandamanaji wameweka vizuizi barabarani.

Siku ya Jumatano jioni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito wa kukomesha mara moja ukandamizaji nchini Burma.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.