Pata taarifa kuu
MYANMAR

Burma yaendelea kukumbwa na maandamano, jeshi lajaribu kukabiliana na waandamanaji

Mamia ya maelfu ya waandamanaji wameendelea kujikusanya katika miji kadhaa ikiwa ni siku ya tisa mfululizo kupinga mapinduzi ya kijeshi nchini Burma.

Hofu yatanda kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa vurugu zaidi nchini Myanmar.
Hofu yatanda kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa vurugu zaidi nchini Myanmar. Reuters/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Myitkyina, katika jimbo la Kachin, risasi zilisikika wakati vikosi vya usalama vikipambana na waandamanaji, lakini kufikia sasa haikuthibitika ikiwa ni risasi za mpira au za moto zilizotumika kuwatawanyisha waandamanaji.

Hata hivyo baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na waandishi wa tatu wa habari wamekamatwa na vikosi vya jeshi.

Vyanzo kadhaa nchini Burma vimethibitisha kwamba mawasiliano ya intaneti yamezimwa kwa muda wa saa tisa kuanzia saa saba mpaka saa tatu majira ya saa za Burma.

Aung San Suu Kyi na serikali yake ilipinduliwa na jeshi Februari 1 kufuatia matokeo ya uchaguzi wa Novemba, ambayo yalikipa ushindi chama chake.

Burma ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi kuanzia mwaka 1962 mpaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.