Pata taarifa kuu
MYANMAR

Burma: Viongozi wa mapinduzi waachilia huru zaidi ya wafungwa 23,000

Wanajeshi walioko madarakani nchini Burma tangu mapinduzi ya Februari 1 wameagiza kuachiliwa kwa wafungwa zaidi ya 23,000 leo Ijumaa, Februari 12, baada ya kukamatwa katika siku za hivi karibuni wakilenga ndugu na washirika wa karibu wa kiongozi wa serikali aliyeondolewa Aung San Suu Kyi na maafisa wa uchaguzi.

Aliyekuwa kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi
Aliyekuwa kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Msamaha kwa wafungwa wengi ili kuondoa msongamano katika jela zilizojaa watu ni kawaida hutolewa kwa tarehe muhimu katika kalenda ya Burma. Leo Ijumaa ni likizo kwa wananchi wote nchini.

Imeripotiwa kuwa Suu Kyi bado amewekwa kwenye kizuizi cha nyumbani na hajaonekana hadharani tangu kutokea mapinduzi zaidi ya wiki moja iliyopita.

Wiki hii rais wa Marekani Joe Biden aliidhinisha agizo la watendaji kuweka vikwazo kwa viongozi wa mapinduzi ya Myanmar.

Hatua hizo zilichuliwa dhidi ya viongozi wa jeshi, familia zao na wafanyabiashara wanaohusishwa nao.

Hatua pia zilichukuliwa kuzuia jeshi kuzipata fedha kiasi cha dola bilioni 1 pesa za serikali zinazoshikiliwa na Marekani.

Wanajeshi walichukua udhibiti tarehe 1 Februari baada ya uchaguzi mkuu ambao Chama cha NLD kilishinda kwa kishindo.

Vikosi vya wanajeshi viliunga mkono upinzani, ambao walikuwa wakidai marudio ya zoezi la kura, wakidai kuwa kulikuwepo na udanganyifu

Mapinduzi yalifanywa wakati kikao kipya cha bunge kilipangwa kufunguliwa.

Bi Suu Kyi yuko chini ya kizuizi cha nyumbani na ameshtakiwa huku maafisa wengine wengi wa NLD pia wamewekwa kizuizini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.