Pata taarifa kuu
MYANMAR

Makao makuu ya chama cha NLD yavamiwa na jeshi Burma

Kundi la wanajeshi limevamia ofisi za makao makuu ya chama cha National League of Democracy (NLD) cha Aung San Suu Kyi, kulingana na chama hicho. Burma inaendelea kukabiliwa na maandamano ya kutaka kiongozi huyo na wenzake waachiliwe huru mara moja bila masharti.

Wanajeshi wavamia makao makuu ya chama cha Aung San Suu Kyi, NLD
Wanajeshi wavamia makao makuu ya chama cha Aung San Suu Kyi, NLD REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Uvamizi huo ulifanyika wakati wa amri ya kutotoka nje ya nchi nzima usiku, ambayo huchukua saa mbili usiku mpaka saa kumi alfajiri 04:00 kwa saa za nchi hiyo, chama cha LND kimeongeza

Bi Suu Kyi hajaonekana tangu mapinduzi ya mapema wiki iliyopita. Serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu watano. Lakini maandamano bado yanaendelea nchini humo.

Kumekuwa na ripoti na video nyingi ambazo hazijathibitishwa zinazoonesha maafisa wa polisi wakivuka ili kujiunga na waandamanaji. Katika maeneo mengine, polisi pia waliripotiwa kuwaruhusu waandamanaji kupita kwenye vizuizi vyao.

Wanajeshi walichukua mamlaka ya nchi tarehe 1 Februari baada ya uchaguzi mkuu ambao chama cha Bi Suu Kyi cha National League for Democracy (NLD) kilishinda kwa kishindo. Jeshi linasema lilichukuwa hatua hiyo kwa lengo la usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.