Mapinduzi Myanmar: Polisi yakabiliana na waandamanaji Naypyidaw
Vikosi vya usalama vimetumia maji kujaribu kuzima maandamno ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi ya kijeshi huko Naypyidaw, mji mkuu wa Burma leo Jumanne, kulingana na picha zilizorushwa moja kwa moja kwenye runinga.
Imechapishwa:
Kundi hili dogo la waandamanaji lilikataa kutawanyika mbele ya kizuizi cha polisi, huku wakipiga kelele na kusema "acheni udikteta wa kijeshi".
Maandamano haya yameingia kwa siku ya nne mfululizo leo Jumanne. Waandamanaji wanaendelea kuomba kiongozi wa chama cha LND Aung San Suu Kyi na viongozi wengine wa chama hiki waachiliwe huru mara moja
Siku ya Jumapili, maandamano, makubwa zaidi tangu maandamano kiraia ya mwaka 2007 yaliyokandamizwa vibaya na jeshi, yalifanyika bila kusababisha hasara kubwa.