Pata taarifa kuu
MYANMAR

Burma: Maelfu ya waandamanaji wamiminika mitaani Yangon dhidi ya mapinduzi

Maelfu ya raia nchini Myanmar (Burma) ameingia mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo, Yangon, leo Jumamosi kupinga mapinduzi yaliyomuondoa mamlakani Aung San Suu Kyi mapema wiki hii, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Vikosi vya usalama nchini Myanmar vikipiga doria.
Vikosi vya usalama nchini Myanmar vikipiga doria. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

"Tunapinga udikteta wa kijeshi," wamesema waandamanaji, ambao wameonekana wakipeperusha bendera nyekundu, rangi ya chama NLD cha cha kiongozi huyo wa zamani. Haya ni maandamano makubwa tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi Jumatatu wiki hiii.

Siku ya Jumatatu, jeshi nchini Myanmar lilitangaza kwamba litashikilia uongozi kwa muda wa mwaka mmoja na kuishtumu serikali ya kiongozi Aung San Suu Kyi kwa kukosa kuchunguza madai ya wizi wa kura katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Hayo yanajiri wakati Waziri mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yassin na rais wa Indonesia Joko Widodo, wameelezea wasiwasi kuhusu mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kuwataka mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia kuandaa mkutano maalumu kuzungumzia suala la kudumisha uthabiti wa kisiasa katika eneo hilo.

Baada ya mkutano na rais Widodo mjini Jakarta, Yassin amesema kuwa mataifa hayo mawili yanafuatilia kwa makini hali ya kisiasa nchini Myanmar na kwamba hali ilivyo nchini humo ni hatua moja nyuma katika mchakato wa mpito wa kidemokrasia.

Siku ya Alhamisi, Baraza la Usalama la umoja wa mataifa lilitoa wito kwa maafisa wa jeshi nchini Myanmar kumwachilia Aung San Suu Kyi na viongozi wengine waliowekwa kizuizini licha ya kwamba hawakukemea mapinduzi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.