Pata taarifa kuu
MYANMAR

Mtandao wa Facebook wazimwa Myanmar

Nchi ya Myanmar, imetanga kuufunga mtandao wa kijamii wa Facebook, ikiwa ni siku chache tu kupita tangu wanajeshi waipindue serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Logo ya mtandao wa kijamii wa Facebook
Logo ya mtandao wa kijamii wa Facebook REUTERS/Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Maofisa nchini humo wanasema kufungiwa kwa mtandao huo wa kijamii ambao kwa mamilioni ya raisa wa Myanmar ndio wamekuwa wakiutegemea kwa mawasiliano, kunalenga kulinda usalama na hali ya utulivu ya taifa hilo.

 

Kiongozi wa kiraia, Aung San Suu Kyi, alikamatwa na wanajeshi punde tu baada ya kutekeleza mapinduzi hayo na tayari wamemfungulia mashtaka.

 

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa mapinduzi ya siku ya Jumatatu hayasimami.

 

Karibu nusu ya raia wa Myanmar ambao ni sawa na watu karibu milioni 58, wanatumia mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo kwa kutochapisha picha ama video, raia wamekuwa wakitumia bure na hivyo kwa wengi matumizi mengine ya tovuti hawafahamu sana.

 

Katika siku chache zilizopita, wanaharakati wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu, wamekuwa wakiutumia mtandao wa Facebook kuhamasisha maandamano ya kupinga mapinduzi hayo.

 

Kampuni ya Facebook imekiri mtandao wao kuwa na tatizo nchini Myanmar na kutoa wito kwa mamlaka za nchi hiyo kurejesha huduma hiyo ili watu waweze kuwasiliana na familia zao na marafiki.

 

Wizara ya mawasiliano nchini humo imesema mtandao wa Facebook utafungwa hadi tarehe 7 ya mwezi huu.

 

Jeshi ambalo tayari limetangaza hali ya dharura nchi nzima kwa muda wa mwaka mmoja, limejaribu kutetea hatua yake kwa madai kuwa uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka jana uligubikwa na udanganyifu, ambapo chama cha Suu Kyi, kilipata ushindi wa zaidi ya asilimia 85, huku vyama vyenye uhusiano na wanajeshi vikishindwa vibaya.

 

Hadi sasa sio Augn San Suu Kyi wala rais Win Myint, wameonekana hadharani tangu kufanyika kwa mapinduzi hayo.

 

Juma hili pia baraza la usalama la umoja wa Mataifa lilijaribu kuandaa azimio kulaani mapinduzi hayo lakini nchi ya China ilitumia kura yake ya Turufu kuzuia kupitishwa kwa azimio lolote. China ikiwa mshirika wa karibu wa wanajeshi wa taifa hilo,

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.