Pata taarifa kuu
BURMA

Jeshi lafanya mapinduzi Myanmar, Aung San Suu Kyi ashikiliwa

Jeshi nchini Myanmar, limefanya mapinduzi na kumkamata kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi, pamoja na viongozi wengine wa juu kwenye Serikali yake na chama chake.

Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye sasa anashikiliwa na jeshi.
Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye sasa anashikiliwa na jeshi. REUTERS/Ann Wang
Matangazo ya kibiashara

Jeshi tayari limetangaza mwaka mmoja wa hali ya dharura nchi nzima, huku likimteua mkuu wake wa majeshi, kuongoza Serikali.

Mamlaka yote yamekabidhiwa kwa jeshi, televisheni ya kijeshi imeripoti.

Mapinduzi haya yamefanyika ikiwa ni siku chache tu tangu chama cha Suu Kyi NLD, kipate ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Katika barua yake aliyoiandika saa chache kabla ya kukamatwa, Suu Kyi amewataka wafuasi wake kutokubali kilitendo cha jeshi, akisema kinarudisha nchi hiyo katika utawala wa mabavu.

Myanmar ambayo pia inafahamika kama Burma, ilikuwa ikiongozwa kijeshi hadi mwaka 2011, ambapo kulifanyika mabadiliko yaliyochochewa na Aung Sann Suu Kyi na kumaliwa utawala wa kijeshi.

Marekani imekashifu mapinduzi hayo, ikisema "Marekani inakataa jaribio lolote la kujaribu kupindisha demokrasia na kubadili matokeo ya uchaguzi yanayorudisha nyuma maendeleo ya taifa hilo".

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amewataka wanajeshi kumuachia kiongozi huyo, wanaharakati na watu wengine wanaoshikiliwa kinyume cha sheria.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, pia amekashifu mapinduzi hayo akiwataka wanajeshi kurejesha mamlaka kwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.