Pata taarifa kuu
WHO

Timu ya WHO yafanya mazungumzo na wanasayansi wa China

Wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanaohusika na kuchunguza asili ya janga la COVID-19 wameanza kukutana na wanasayansi wa China leo Ijumaa na wanatarajiwa kuzuru maabara na hospitali huko Wuhan, eneo kunakoshukiwa kuzuka virusi vya Corona, katikati mwa China.

Nembo ya WHO
Nembo ya WHO Fabrice Ciffrini / AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Shughuli hi ilianza baada ya kumalizika Alhamisi ya kipindi cha siku kumi na nne wakati ambapo wanasayansi wa kimataifa walilazimika kujiweka karantini katika hoteli moja kama tahadhari ya kiafya walipowasili Wuhan, mji ambao kesi ya kwanza ya virusi vya Corona iligunduliwa mwishoni mwa mwaka 2019.

Wakati wanatarajia kubaki nchini China kwa muda wa wiki mbili zaidi, wataalam hao wanapanga kuzuru soko moja jijini Wuhan leo Ijumaa linalochukuliwa kuwa chanzo cha kwanza cha mlipuko wa Corona, WHO imesema.

Kisha watazuru Taasisi ya Virolojia ya Wuhan. Kulingana na nadharia moja, iliyokanushwa na China, janga hilo lilisababishwa na ukiukaji wa maabara hii ya serikali.

"Mkutano wa kwanza wa ana kwa ana na wenzetu. Marekebisho: kuvaa barakoa, kwa sababu ya vizuizi vya matibabu. Tunazungumzia mpango wa ziara yetu," Marion Koopmans, mtaalam wa virolojia katika taasisi ya Uholanzi amesema kwenye Twitter leo Ijumaa.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.