Pata taarifa kuu
IRAN-ISRAEL

Iran yaishtumu Israel kwa kuhusika katika mauaji ya mwanasayansi wake mkuu

Iran imeinyooshea kidole cha lawama Israel kuhusika katika mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkuu wa nyuklia na mwanajeshi Iran, na kuahidi kulipiza kisasi kwa wale waliohusika na mauaji hayo.

Picha ndogo ikimuonesha mwanasayansi wa Iran, Mohsen Fakhrizadeh, aliyeuawa katika shambulio siku ya Ijumaa
Picha ndogo ikimuonesha mwanasayansi wa Iran, Mohsen Fakhrizadeh, aliyeuawa katika shambulio siku ya Ijumaa AP Photo
Matangazo ya kibiashara

Mohsen Fakhrizadeh aliuawa katika operesheni ya kushangaza Kaskazini mwa Tehran. Kwanza gari ndogo lililipuka barabarani, mbele ya gari lake, kabla ya kushambuliwa kwa risasi.

 

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, ameishutumu moja kwa moja Israel kwa kuhusika katika mauaji hayo.

 

Jina la Mohsen Fakhrizadeh lilitajwa mnamo mwezi Aprili 2018 na Waziri Mkuu wa Israeli katika hotuba yake kwenye televisheni. Benyamin Netanayhu alimshtumu kuwa mmoja wa maafisa wakuu wa mpango wa nyuklia wa Tehran. "Kumbukeni vizuri jina hili: Fakrizadeh", Bw. Netanyahu alisema wakati huo.

 

Mwanasayansi huyo mwandamizi pia alikuwa kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.

 

Katika siku za hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Israel ameendelea kuweka wazi wasiwasi wake kuona serikali ijayo ya Biden inachukuwa msimamo wa wazi kwa mazungumzo na Iran kuliko utawala wa Trump, ameripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Guilhem Delteil.

 

"Hatupaswi kurudi kwenye makubaliano ya mwaka 2015," Waziri Mku wa Israel alisema siku ya Jumapili katika ujumbe wa wazi kwa rais wa mteule wa Marekani. Benjamin Netanyahu amekuwa akipambana dhidi ya makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.