Pata taarifa kuu
JAPANI-MAFURIKO-USALAMA

Zaidi ya thelathini na sita waangamia kufuatia mafuriko Japan

Juhudi za kuwatafuta  watu waliotoweka baada ya kutokea kwa maparomoko ya ardhi na mafuriko yaliyozuka katika Jimbo la Kumamoto nchini  Japan kufuatia mvua kubwa inayonyesha, zinaendelea.

Karibu watu 40 wanaaminika wamekufa wakati mvua kubwa zinaendelea kunyesha kwenye kisiwa cha Kyushu Kusini mwa Japani.
Karibu watu 40 wanaaminika wamekufa wakati mvua kubwa zinaendelea kunyesha kwenye kisiwa cha Kyushu Kusini mwa Japani. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Japan, watu zaidi ya 36 wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia janga hilo lilitokea siku ya Jumamosi baada ya mito kuvunja kingo  kwenye maeneo ya mabonde.

Karibu watu 40 wanaaminika wamekufa wakati mvua kubwa zinaendelea kunyesha kwenye kisiwa cha Kyushu Kusini mwa Japani, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi tayari yamesababisha vifo vya watu 21, watu 18 wanaaminika kuwa wamekufa na 13 wamekosekana waliko, katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri Yoshihide Suga ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari.

Amesema kuwa vituo vya uokoaji vilivyowekwa pia vinaheshimu hatua za usafi zinazohitajika ili kuzuia janga la Corona.

Siku ya Jumamosi, watu 200,000 waliombwa kuondoka katika nyumba zao, kulingana na shirika la habari la Kyodo.

Mwezi Oktoba mwaka jana, mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Hagibis yaliua watu 90.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.