Pata taarifa kuu
UINGEREZA-CHINA-SIASA-USALAMA-USHIRIKIANO

London kuwarahisishia wahamiaji kutoka Hong Kong

Uingereza iko tayari kubadilisha sheria zake za uhamiaji ikiwa China itaweka sheria mpya ya usalama wa kitaifa huko Hong Kong, amesema Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mahojiano yaliyo chapishwa na Gazeti la South China Mornin Post Jumatano Asubuhi.

Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson aionya china kuhusu sheria yake usalama wa kitaifa Hong Kong
Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson aionya china kuhusu sheria yake usalama wa kitaifa Hong Kong REUTERS/Lisi Niesner
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uingereza, inaona kuwa uamuzi wa Beijing wa kuweka sheria ya usalama wa kitaifa huko Hong Kong utaathiri uhuru na kupunguza mamlaka ya kujitawala kwa jimbo hilo.

Ikiwa China itaendelea na mpango wake, serikali ya Uingereza itabadilisha sheria zake za uhamiaji, amesema Johnson.

Wakaazi wa Hong Kong wanaotumia pasipoti ya Uingereza (BNO) wataweza kuingia nchini Uingereza kwa kipindi cha miezi 12 ambacho kitaongezwa na kuwa na haki za ziada, pamoja na kuruhusiwa kupata ajira, "hali ambayo inaweza kuwapa haki kama raia wa Uingereza, " ameongeza Waziri Mkuu wa Uingereza.

Karibu wakazi 35,000 wa Hong Kong hivi sasa wanatumia pasipoti hiyo na wengine milioni 2 wana haki ya kuiombea na kupewa, kiongozi huyo wa Uingereza amebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.