Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-USALAMA

Pyongyang yaanza kuvunja mitambo yake ya nyuklia

Picha za Satellite zinaonyesha kwamba Korea Kaskazini imeanza kuvunja miundombinu muhimu kwenye maeneo kunakofanyika majaribio ya makombora ya masafa marefu, kituo cha wataalam kimetangaza.

Kwa mujibu wa 38 North, picha za kuanzia Julai 20 zinaonyesha shughuli za kuvunjwa kwajengo kwenye eneo ambako satellites za Sohae zinakorushwa, katika pwani ya magharibi ya Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa 38 North, picha za kuanzia Julai 20 zinaonyesha shughuli za kuvunjwa kwajengo kwenye eneo ambako satellites za Sohae zinakorushwa, katika pwani ya magharibi ya Korea Kaskazini. REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ni ishara kwamba Pyongyang inapiga hatua kuelekea kutachana na mpango wake nyuklia.

"Kutokana na kwamba mitambo hii ilikuwa na jukumu muhimu katika maendeleo ya teknolojia kwa mpango wa Korea Kaskazini, juhudi hizi zinaonysha hatua muhimu ya matumaini kwa Korea Kaskazini," kundi la wakaguzi nchini Korea Kaskazini ( 38 North) lenye makao yake makuu mjini Washington limeandika kwenye ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa 38 North, picha za kuanzia Julai 20 zinaonyesha shughuli za kuvunjwa kwajengo kwenye eneo ambako satellites za Sohae zinakorushwa, katika pwani ya magharibi ya Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema baada ya mkutano wa kihistoria Juni 12 na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwamba Kim alikuwa ameahidi kuwa eneo kuu la majaribio ya makombora ya masafa marefu litaharibiwa hivi karibuni.

Ripoti ya 38 North inakuja wakati ambapo maswali yanaendelea kuongezeka kuhusu nia ya Pyongyang ya kuachana na mipango yake ya makombora ya masafa marefu na nyuklia na kujikita katika kuleta amani katika rasi ya Korea, kama ilivyoahidiwa katika mkutano wa kilele wa Singapore mwezi uliopita.

Afisa wa Korea Kusini amesema Jumanne wiki hii kwamba ikulu ya Blue House mjini Seoul imefahamishwa na idara ya ujasusi kuhusu kuvunjwakwa kambi ya Sohae, bila kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.