Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Rouhani: Iran ina haki ya kurutubisha uranium kwa madhumuni ya "amani"

Serikali ya Iran imesema kuwa itaendelea na mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium. Viongozi wa Iran wanasema ni haki ya Iran kuwa na teknolojia ya Kinyuklia kwa madhumuni ya amani.

Rais wa Iran Hassan Rouhani anasem anchi yake itaendelea na mpango wa kurutubisha madini ya uranium kwa madhumuni ya amani..
Rais wa Iran Hassan Rouhani anasem anchi yake itaendelea na mpango wa kurutubisha madini ya uranium kwa madhumuni ya amani.. HO / IRANIAN PRESIDENCY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran ina haki ya kuimarisha madini ya uranium kwa madhumuni ya "amani", Rais wa Irani Hassan Rohani amesema Jumanne wiki hii.

Jamhuri ya Kiislamu ilitangaza hapo awali kuwa inaweza kuendelea na mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium kufikia asilimia 20, jambo ambalo ni marufuku kulingana na mkataba wa Vienna wa mwezi Julai kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Katika hotuba yake leo Jumanne, rais wa Irani pia amesema kuwa uamuzi wa Donald Trump wa kuitoa Marekani kwenye makubaliano ya Vienna mnamo mwezi Mei ni "wa kusikitisha na kinyume cha sheria" na kwamba amepoteza hadhi ya Marekani duniani kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.