Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Macron amhimiza Rouhani kushiriki mazungumzo mapya kuhusu Nyuklia

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezungumza na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani na kumhimiza kukubali kushiriki katika mazungumzo mapya kuhusu mradi wake wa Nyuklia.

Rais wa Iran Hassan Rohani amkumbusha Macron kwamba mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia yamekwisha
Rais wa Iran Hassan Rohani amkumbusha Macron kwamba mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia yamekwisha ADEM ALTAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, rais Rohani amemwambia rais Macron kupitia mazungumzo ya simu kuwa, mkataba uliopo uliotiwa saini kati ya nchi yake na mataifa ya Magharibi hauwezi kujadiliwa tena.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuamua mwezi ujao iwapo ataendelea kuunga mkono mkataba huo ambao unaitaka Iran kutoendelea na mradi huo kwa muda wa miaka 10 ijayo.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ambaye amezuru Israel amesema, Iran inaendelea kutishia usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo na Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu, Tel Aviv tarehe 29 Aprili.
waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo na Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu, Tel Aviv tarehe 29 Aprili. Thomas Coex/Pool via Reuters

Pompeo ameeleza kuwa, hili limedhihirisha kutokana na serikali ya Tehren kumuunga mkono rais wa Syria Bashar Al Asaad na waasi wa Kihouthi nchini Yemen.

Aidha, amesisitiza kuwa Marekani inaendelea kutilia shaka mkataba wa Nyuklia wa Iran ambao ulikubaliwa kuwa nchi hiyo isitishe mradi wake kwa angalau miaka 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.