Pata taarifa kuu
CHINA-MLIPUKO-USALAMA

Milipuko mikubwa yatokea Tianjin, kaskazini mwa China

Mji wa bandari wa Tianjin, karibu na Beijing, kaskazini mwa China, umekumbwa Alhamisi Agosti 13 na milipuko mikubwa katika eneo la viwanda, ambapo sababu bado hazijajulikani. Kwa uchache watu 17 wamepoteza maisha na zaidi ya 400 kwa sasa wamelazwa hospitalini.

Magari yamechomwa moto baada ya milipuko katika wilaya ya Binhai katika mji waTianjin, China.
Magari yamechomwa moto baada ya milipuko katika wilaya ya Binhai katika mji waTianjin, China. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Milipuko hiyo ilitokea saa 3:30 usiku saa za China (sawa na saa 10:30 jioni saa za kimataifa). Ni chombo kilichokua kimejaa vilipuzi ambacho kiliwaka moto kwa sababu zisiojulikana. Ajali hiyo imetokea katika bandari ya viwanda ya Tianjin, moja ya bandari kubwa nchini humo, katika sehemu ambapo kulikua kumehifadhiwa bidhaa hatari na zenye kushika moto kwa haraka. Kulikuwa na milipuko mikubwa miwili ambayo ilipelekea mji huo wa bandari wa Tianjin kufunikwa na wingu kubwa la moto na vumbi, huku kelele nyingi zikisikika, wamesema mashahidi.

Wimbi la mshtuko limepasua majengo yalioko pembezoni mwa eneo hilo la viwanda na limerekodiwa na chombo cha seismographs katika ukubwa wa 2.9 richter, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Shanghai, Delphine Sureau. Kwa mujibu wa akaunti iliothibitishwa ya mtandao wa kijamii kutoka China wa Weibo wa kituo cha mitandao inayochunguza tetemeko, ukubwa wa mlipuko wa kwanza ulikua sawa na mpasuko wa tani tatu za TNT, wakati mlipuko wa pili ulikuwa na nguvu sawa na ile ya tani 21 ya kifaa hicho kiliolipuka.

Moto uliosababishwa na mlipuko huo kwa sasa umedhibitiwa, vyombo vya habari nchini China vimebaini, lakini viongozi wamepoteza mawasiliano na wazima moto waliotumwa katika eneo la tukio. Majengo kadhaa hayana huduma ya umeme. Wakaazi wa mji huo wameyahama makaazi yao kwa sababu wanahofu kuwa huenda mlipuko huo kusababisha uvujaji wa gesi katika majengo yalioathirika. Haijajulikana chanzo cha moto huo, lakini inaaminika kuwa nia ajali, ambayo imesababishwa na uzembe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.