Pata taarifa kuu
JAPAN-HIROSHIMA-KUMBUKUMBU

Shambulio la Hiroshima lakumbukwa Japan

Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima, na siku tatu baadae mjini Nagasaki.

Raia wa japan waadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya mlipuko wa bomu la Atomiki katika mji wa Hiroshima, Agosti 6, 2015.
Raia wa japan waadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya mlipuko wa bomu la Atomiki katika mji wa Hiroshima, Agosti 6, 2015. REUTERS/Toru Hanai
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la bomu lililodondoshwa katika mji wa Hiroshima liliwaua maelfu ya raia. Ilikua tarehe 6 Agosti mwaka 1945.

Wakati bomu hilo la atomiki liliporushwa na ndege ya kivita ya Marekani B-29 Enola Bay, ambayo ilikua ikiruka kwenye umbali wa juu wa mita 600 kutoka ardhini katika anga la mji wa Hiroshima, wakaazi 300,000 wa mji huo walijikuta hawana makaazi kufuatia mlipuko wa bomu hilo.

Takriban watu laki moja na arobaini walipoteza maisha. Watu elfu sabini na tano walifariki papo hapo baada ya ndege ya Marekani kudondosha bomu hilo la atomiki, huku watu wengine hamsini walifariki kutokana na athari za mionzi ya sumu, na wengine zaidi ya 200,000 walijikuta walipoteza baadhi ya viungo vyao vya mwili, na wengi walipoteza ajira na wengine kushindwa kufunga ndoa kutokana na ulemavu ambao waliendelea kuupata kufuatia sumu ya bomu hilo la atomiki lililodondoshwa katika mji wa Hiroshima.

Akilihutubia taifa, Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima inaonesha jinsi gani jitihada zinatakiwa kufantwa katika kupiga vita matumizi ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.