Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-AJALI-USALAMA

Korea Kusini : mwaka mmoja baada ya kuzama kwa Ferry " MV Sewol"

Raia wa Korea Kusini wanaadhimisha mwaka mmoja kukumbuka ajali ya kuzama kwa Ferry iliyosababisha watu 300 kupoteza maisha.

Ndugu na jamaa wa waathirika wa ajali ya " MV Sewol" wamejielekeza katika eneo la tukio, mwaka mmoja baada ya ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 304, Aprili 15 mwaka 2015.
Ndugu na jamaa wa waathirika wa ajali ya " MV Sewol" wamejielekeza katika eneo la tukio, mwaka mmoja baada ya ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 304, Aprili 15 mwaka 2015. REUTERS/Jeon Heon-Kyun/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea katika kisiwa cha Jindo, na idadi kubwa ya waliopoteza maisha walikuwa ni wanafunzi 250 waliokuwa ndani ya ferry hiyo wakiwa katika ziara ya elimu.

Wizara ya Mambo ya ndani imesema mashirika 300 yasiyo ya kiserikali na serikali za mitaa kote nchini wanaadhimisha siku hii.

Familia za waliopoteza maisha tayari wamefika katika eneo la ajali hiyo na wengi kuangua kilio walipokumbuka ajali hiyo ilivyotokea.

Serikali ya Korea Kusini imeshtumiwa kwa kuendelea kupuuza usalama wa safari za majini na kutofanya upekuzi wa mara kwa mara wa vyombo vya safari za majini.

Ni watu 100 ndio waliokoloewa wakati wa ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.