Pata taarifa kuu
UMOJA WA FALME ZA KIARABU, UBUNIFU-USALAMA

Ndege inayotumia umeme jua yazunguka ulimwengu

Wabunifu wa ndege hiyo inayotumia umeme jua kama mafuta wametoa muda wa siku tano kwa ndege hiyo kuwa itakua imekamilisha safari yake ya kuuzunguka ulimwengu.

Solar Impulse 2 ikipaa juu ya Msikiti katika mji wa Abu Dhabi, Februari 26, 2015, katika maandalizi  ya safari yake ya kuuzunguka ulimwengu.
Solar Impulse 2 ikipaa juu ya Msikiti katika mji wa Abu Dhabi, Februari 26, 2015, katika maandalizi ya safari yake ya kuuzunguka ulimwengu. REUTERS/Solar Impulse/Revillard
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo inayojulikana kwa jina la Solar Impulse 2 inatazamiwa kutua katika vituo kumi na mbili katika safari yake hiyo ukianzia kwenye hatua yake ya kwanza ya kuruka hewani katika mji wa Abu Dhabi.

Ndege hiyo imeanza safari yake ya kuuzunguka ulimwengu Jumatatu wiki hii, na inatumia nishati ya jua kupitia vifaa vya kunasa mionzi ya jua vilivyowekwa kwenye mabawa yake.

Ndege hiyo ina kiti kimoja na mabawa yenye ukubwa wa jimbo la jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari.

Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku.

Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.