Pata taarifa kuu
PAKISTAN-CHARLIE HEBDO-MAANDAMANO-JAMII-Usalama

Maandamano makubwa dhidi ya Charlie Hebdo

Maandamano makubwa dhidi ya Charlie Hebdo yamesababisha watu wawili kujeruhiwa nchini Pakistan, ikiwa ni pamoja na mpiga picha kutoka shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kama Lahore siku moja kabla (picha), mamia ya waandamanaji waliingia mitaani katika mji wa Karachi leo Ijumaa, Januari 16 dhidi ya kuchapishwa kwa katuni ya Mtume Muhammad.
Kama Lahore siku moja kabla (picha), mamia ya waandamanaji waliingia mitaani katika mji wa Karachi leo Ijumaa, Januari 16 dhidi ya kuchapishwa kwa katuni ya Mtume Muhammad. REUTERS/Mohsin Raza
Matangazo ya kibiashara

Mpiga picha huyo amekua katika kazi yake ya kila siku, akijaribu kupiga picha makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, ambao wamekua wamekuja kuonyesha hasira zao dhidi ya kuchapishwa kwa katuni ya Mtume Muhammad.

Makundi kadhaa ya watu kutoka jamii ya Waislam yametolea wito ndugu zao katika imani kuingia barabarani, baada ya sala kuu ya Ijumaa Januari 16, ili kulaani toleo jipya la jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo, ambapo kwenye ukurasa wake wa kwanza kumechapishwa katuni ya Mtume Muhammad. Katika mji wa Karachi, mamia ya watu waliitikia wito huo.

Wengine wametaka kuandamana hadi kwenye ubalozi mdogo wa Ufaransa. Makabiliano yalizuka kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji hao wakati ambapo polisi ilijaribu kuzuia maandamano hayo kwa kufyatua risasi hewani na kuwapulizia maji waandamanaji.

Kama ilivyo mahali pengine katika ulimwengu wa Kiislamu, kuchapishwa kwa katuni ya Mtume Muhammad, kulizua hali ya taharuki nchini Pakistan.

Jana Alhamisi Januari 15, Bunge kwa kauli moja lilipitisha azimio la kulaani uchapishaji wa katuni hilo, likisema kwamba uhuru wa kujieleza usitumike kwa kuzikosea imani za kidini.
Kufuru inaadhibiwa nchini Pakistan. Matusi dhidi ya Mtume Mohammed ni adhabu ya kifo.

Jumanne Januari 13, zaidi ya waandamanaji hamsini walikusanyika pia katika mji wa Peshawar kwa kutoa heshima kwa watu waliohusika katika mauaji yaliyotokea kwenye makao makuu ya jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo. " Mashujaa", "wamekufa mashahidi" kwa " kusitisha kufuru", walisema waandamanaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.