Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-Sheria-haki za binadamu

Korea Kusini: nahodha wa meli ya Sewol ahukumiwa kifungo cha miaka 36 jela

Kufuatia kesi iliyodumu miezi mitano huku manusura wakitoa ushahidi wao wa kutosha kuhusu kuzama maji kwa meli iliyokua ikibeba abiria 476, wakiwemo wanafunzi 250, hatimaye hukumu imetolea. katika ajali hiyo watu 304 walikufa maji baada ya meli waliyokua emo kuzama maji.

Nahodha wa meli ya Sewol, Lee Joon-Seok (akivalia nguo za kijani pamoja na miwani, wa kwanza kulia) akizunguukwa na wasaidizi wake, wakati wa Mahakama ipokua ikito hukumu, Novemba 11 mwaka 2014, Gwangju.
Nahodha wa meli ya Sewol, Lee Joon-Seok (akivalia nguo za kijani pamoja na miwani, wa kwanza kulia) akizunguukwa na wasaidizi wake, wakati wa Mahakama ipokua ikito hukumu, Novemba 11 mwaka 2014, Gwangju. REUTERS/Ed Jones/Pool
Matangazo ya kibiashara

Nahodha wa meli hiyo amehukumiwa kifungo cha miaka 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya uzembe wa kikazi na kusababisha vifo. Lee Joon-Seok, mwenye umri wa miaka 70, alikua anakabiliwa na adhabu ya kifo. Nahodha huyo aliwasihi abiria kutoondoka ndani ya meli wakati chombo hicho kilikua kikizama. Lakini baada ya kuzama kwa meli hiyo, nahodha huyo aliondoka mara moja wakati ambapo mamia ya abiria walikua walikwama ndani ya meli.

Hata hivo Ofisi ya mashtaka imekataa rufaa. Ofisi ya mashtaka imesema haikubaliani na adhabu aliyopewa Lee Joon-Seok na wasaidizi.

Tuhuma za kuua kutokana na "uzembe uliyokithiri" ambazo Ofisi ya mashtaka ilikua ikimtuhumu na kumuombea adhabu ya kifo, zilifutwa na majaji watatu ya Mahakama ya Gwangju. Wafanyakazi wengine kumi na moja waliyokua wakihudumu katika meli hiyo wamepewa adhabu tofauti ya kifungo jela.

Baadhi ya familia za wanafunzi hao zilizohudhuria kesi hiyo zilionyesha hasira zao kuona Lee Joon-Seok hakupewa adhabu ya kifo, ambayo hata hivyo haijawahi kutumika Korea kusini tangu mwaka 1997. " Haki ikowapi? ", mwanamke mmoja amewauliza majaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.