Pata taarifa kuu

Kiongozi wa kijeshi Korea Kaskazini aondolewa katika nafasi yake

Kiongozi wa kijeshi wa Korea Kaskazini ambaye anatajwa kuwa ni mjomba wa kiongozi wa taifa hilo ameondolewa katika wadhifa wake aliokuwa akiushikilia,vyombo vya habari vya Korea Kusini vimearifu.

Kiongozi wa bodi ya Jeshi la Korea Kaskazini Chang Song-taek
Kiongozi wa bodi ya Jeshi la Korea Kaskazini Chang Song-taek
Matangazo ya kibiashara

Chang Song-Thaek, mwenye umri wa miaka 67, amepoteza nafasi yake ya makamu mwenyekiti wa bodi ya kijeshi nchini humo.

Kama ikithibitishwa, kuondolewa kwa Chang kutakuwa ni mageuzi makubwa katika uongozi wa Korea Kaskazini kwa mujibu wa wachambuzi.

Itakumbukwa kuwa Kim Jong-un aliingia madarakani baada ya kifo cha Kim Jong-il mwaka 2011.

Taarifa za karibuni ziliibuka katika mkutano mfupi wa kiintelijensia iliyokabidhiwa kwa wabunge wa Korea Kusini.

Shirika la ujasusi la taifa hilo (NIS) lilifanya tathimini iliyojikita katika taarifa za vyanzo mbalimbali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.