Pata taarifa kuu
Korea kaskazini

Korea Kaskazini na Kusini zatolewa wito kufikia mwafaka juu ya kufunguliwa kwa eneo la kiviwanda, Kaesong

Wafanyabiashara wa Korea kusini wamezitaka nchi za Korea kaskazini na Korea kusini kuhakikiksha kuwa mpango wa mazungumzo juu ya kufungua tena eneo la kiviwanda la Kaesong unafanikiwa katika awamu hii ya mazungumzo.

Wafanyakazi wa kiwanda cha Viatu kilicho eneo la Kaesong
Wafanyakazi wa kiwanda cha Viatu kilicho eneo la Kaesong REUTERS/Lee Jin-man/Pool/Files
Matangazo ya kibiashara

Wafanyabiashara hao wamesema kuwa Mamlaka ya Korea kaskazini na kusini lazima wafikie muafaka juu ya Mustakabali wa Kaesong kwa kuwa maisha yao yako katika wakati mgumu baada ya kufungwa kwa eneo hilo.

Eneo la Kaesong, lenye viwanda 123 vya korea kusini vilifungwa baada ya Serikali ya Pyongyang kuondoa Wafanyakazi wake 53,000 mwezi Aprili kufuatia kuwepo kwa hali ya Mvutano na vitisho vya mapigano baina ya mataifa hayo mawili.

Awamu sita za mazungumzo hazikuzaa matunda na mazungumzo ya awamu ya saba ya siku ya jumatano inaonekana kuwa nafasi ya mwisho katika jitihada za kupata suluhu.

Juma lililopita , wakati Serikali ya Korea kusini ikitangaza kuwa itaanza kuwalipa fidia wafanyabiashara walioathirika na kufungwa kwa viwanda, Korea kaskazini ikapendekeza kufanya Mazungumzo na Korea kusini.
 

Eneo la Kaesong lilijengwa mwaka 2004 kuashiria ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili, lakini dosari ilianza kuonekana baada ya jaribio la Korea kaskazini la silaha zake za Nuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.