Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI

Korea kusini yaonya kuwa Mazungumzo zaidi na Korea kaskazini yatatoa fursa kwa nchi hiyo kuendelea na Mradi wa Nuklia

Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameonya juu ya kuihusisha Korea kaskazini katika mazungumzo, ambayo amedai kuwa yatatoa nafasi zaidi kwa Pyongyang kuendelea na mradi wake wa kutengeneza silaha za Nuklia.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Matangazo ya kibiashara

Onyo hilo limekuja siku moja baada ya Korea kaskazini kuomba kufanya mazungumzo na Marekani juu ya Mradi wa Nuklia.
 

Washington imeridhia ombi la Pyongyang ikisema kuwa Korea kaskazini haina budi kuonesha ushahidi kuwa wako tayari kuachana na mpango wake wa Nuklia kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo.
 

Korea kaskazini iliingia katika uhasama na Korea kusini na Marekani baada ya kuwepo kwa hali ya kurushiana maneno na vitisho vya kutokea kwa mashambulizi ya kijeshi hasa baada ya Korea kaskazini kufanya jaribio lake la Nuklia.
 

Mazungumzo ya Viongozi wa Korea kaskazini na Marekani yaliyofanyika Mwezi Februari mwaka jana yalikamilika kwa kuwepo kwa makubaliano kwa marekani kutoa msaada wa Chakula kwa sharti kuwa Korea kaskazini iachane na majaribio ya Silaha za Nuklia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.