Pata taarifa kuu
MYANMAR

Watu 20 wapoteza maisha nchini Myanmar katika mapigano ya kidini baina ya Waislamu na Wabudha

Machafuko ya kidini baina ya waumini wa dini ya kiislamu na wale wakibudha nchini Myanmar yamesababisha vifo vya watu ishirini. Hofu ya usalama imezidi kutanda na tayari serikali imetangaza hali ya hatari baada ya kushuhudia mapigano makali baina ya jamii hizo mbili.

Photo: Teza Hlaing / The Irrawaddy
Matangazo ya kibiashara

Takribani malori hamsini ya kijeshi yanapiga doria katika mji huo kukabiliana na wapiganaji ambao wengi wanatumia visu na mapanga, nyumba nyingi na misikiti zimeripotiwa kuharibiwa katika machafuko hayo.

Tangu kuzuka kwa machafuko hayo mwaka uliopita, maelfu ya raia wa Myanmar wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wamekimbia makazi yao na kuishi nchini Malaysia kama wakimbizi .

Umoja wa mataifa UN, Marekani, Uingereza na makundi mbalimbali ya haki za binadamu yametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kufanyika mazungumzo kati ya jamii zinazotofautiana ili kuepusha madhara zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.